Home KITAIFA WAKULIMA WATAKIWA KUTUNZA CHAKULA MARA BAADA YA MAVUNO

WAKULIMA WATAKIWA KUTUNZA CHAKULA MARA BAADA YA MAVUNO

WAKULIMA wanawake nchini wameshauriwa kutunza chakula mara baada ya mavuno ili kupunguza upotevu wa chakula kwa wingi.

Akifunga Mradi wa Supia II Project Learning na Closure Workshop Scalling up Public investments in argriculture (SUPIA II) Unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Tanzania Mjumbe wa Kamati ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum kundi la Vijana Ng’wasi Kamani amesema katika jamii yeyote familia ikikosa chakula aibu humkuta mama huku akiwataka kupata elimu ya utunzaji wa chakula.

‘’Katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tumeahidi tutaendelea kuhakikisha tunapunguza upotevu wa Chakula baada ya mavuno, kaya ikipata njaa anayeaibika ni mama, tunaweza kuwa tunafanya vizuri shabani, tunavuna vizuri lakini tusipopata elimu tunaweza kujikuta tunapoteza chakula kwa wingi sana,’’ amesema Ng’wasi.

Pamoja na hayo amewataka wakulima wanawake kuwa kinara katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kukomboa mazingira ikiwa ni kupanda miti Pamoja na kuachana na mila na desturi na matokeo yake wamiliki ardhi.

Akizungumzia Mradi wa Supia II Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wakulima Wanawake Tanzania Anastazia Madeje amesema Ujio wa mradi huo umewabadilisha Wanawake kwani umewawezesha kushiriki kwa ufanisi katika ngazi mbalimbali za maamuzi na imekuwa rahisi kufuatilia haki zao na kupata ushirikiano mkubwa wa serikali nakuitaka kusimamia kikamilifu viwanda vinavyochakata mbegu za asili hasa cha Dodoma na Singida ili kuendeleza kilimo Ikolojia.

Mkulima kutoka Singida Fredina Makeleja amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata katika mradi huo bado wameitaka Serikali kuendelea kuwatumia katika uchambuzi wa Bajeti ili kujua bajeti inayotengwa inakidhi mahitaji kwa wakulima.

‘’Serikali itushirikishe katika kuandaa mipango ya kukuza kilimo na kuyashirikisha majukwaa ya wakulima kuendeleza mradi ili kuleta matokeo chaya,’’amesema Makeleja.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Actionaid Tanzania Bavon Christopher amesema ufadhili umeisha lakini mradi utaendelea nakuwataka wakulima kufanya kazi kadri ya uwezo wao.

‘’Tusipokuwa makini tunaweza kuwa watumwa katika nchi yetu,tunapozungumzia kilimo hai yapo makampuni makubwa yanahakikisha kwamba yanalichukua soko lote, sisi kama Actionaid Tanzania tutaendelea kuwa sauti yenu siyo katika Nchi lakini hata kimataifa tutaendelea kuyashambulia makampuni makubwa ambayo yanazikandamiza nchi maskini na kuziwekea mifumo tegemezi kwao,’’.

Mradi wa Supia II Project Learning na Closure Workshop Scalling up Public investments in argriculture (SUPIA II) ulianza mwaka 2021 lengo ni kuchechemua uwekezaji katika kilimo.

Previous articleMUUGUZI KCMC AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI UCHOCHORO WA MALINDI
Next articleKATIBU MKUU NISHATI ASISITIZA GST KUFANYA UTAFITI ZAIDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here