Wakulima wameshauriwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa tafiti na taasisi ya utafiti wa kilomo Tanzania (TARI)na zenye tija na kuachana na zile zisizo na ubora ili kuweza kuongeza uzalishaji katika mazao
Hayo yamesemwa na mtafiti mgunduzi wa mbegu za mtama,uwele pamoja na ulezi anayeratibu mazao hayo kitaifa kutoka TARI Emmanuel Mwenda ,katika maonesho ya 30 ya nanenane kanda ya mashariki.
Mwenda amesema mkulima akitumia mbegu zilizofanyiwa tafiti pamoja na kutumia kanuni bora za kilimo mkulima huyo anauwezo wa kuzalisha tani 4 kwa hekta moja.
Kwa upande wake mtafiti wa mazao ya jamii ya mikunde Levocatus Baitwa,amewashauri wakulima kuwekeza katika mazao ya muda mfupi.
Nao wakulima wamewapongeza watafiti wa mbegu za kilimo kwa kuzalisha mbegu zenye tija huku wakiomba watafiti hao kuzalisha mbegu hizo kwa wingi ili ziweze kuwafikia wakulima kwa wakati.