Home KITAIFA WAKULIMA WA KAKAO MBEYA WAASWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUWA...

WAKULIMA WA KAKAO MBEYA WAASWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUWA NA MAAMUZI KATIKA BEI

 

Mbeya

Wakulima wa zao la Kakao mkoani Mbeya wametakiwa kuacha kutengeneza matabaka na badala yake waungane kupitia Vyama vya ushirika ili kuwa na sauti moja itakayo wawezesha kuamua bei nzuri itakayo wanufaisha wanapohitaji kuuza bidhaa hiyo sokoni.

Ushauri huo ulitolewa Mei 26,2023 Wilayani Kyela na kaimu meneja mkuu wa ushirika (KYECU) Julius Mwankenja anayedai kuna baadhi ya wakulima wanauwezo wa kufanya maamuzi lakini wamekuwa wakijitenga na wenzao hali inayowarudisha nyuma.

“Wakulima wakiungana wanakuwa na nguvu tumeona safari hii,licha ya wakulima wengi kuuza bidhaa hiyo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia ushirika lakini hawashiriki kwenye maamuzi ya bei kwakuwa siyo wanachama,” amesema

Julius amesema Ili mkulima uweze kushiriki maamuzi ya kuamua bei kwenye minada wanayofanya kila wiki, nilazima awe mwanachama hai kwenye vikundi vya msingi vya ushirika.

“Tunaona wakulima wengi wanauwezo wa kufanya maamuzi mazuri yatakayoleta tija kwao lakini hawapati fursa hiyo kwakukosa sifa,” amesema

Hoja iliyoungwa mkono na Afisa Ushirika Wilaya ya Kyela,Thadei Mwambeso anayedai kwa sasa serikali inawasikiliza wakulima na kutoa fursa tofauti kwao kupitia Vyama vya ushirika.

“Serikali ikitaka kutoa pembejeo bora na kwa bei na fuu wanaanza kupitia kwenye Vyama vya ushirika hadi wakinufaika wale ndipo wanaanza kuangalia wengine nimuhimu kujiunga,” amesema

Amesema kupitia mfumo huo mazao ya wakulima yanauzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo ndani ya saa 24 mkulima anaanza kupata malipo yake kupitia simu yake.

“Katika mfumo wa stakabadhi ghalani hakuna watu kunyonywa na hata vipimo vinavyotumika ni vya kidigijitali hata pointi chache za mkulima zikibaki anaziona,” amesema

Mkulima wa zao hilo Bruno Benedict amesema kudanganywa na baadhi ya wafanyabiashara ni moja ya sababu zinazochelewesha wakulima wengi kusita kujiunga na Vyama vya ushirika.

“Wamekuwa wakidanganywa lakini tunaomba Mamlaka kuzidi kutoa elimu Kwa wakulima kwani jambo lolote linapoanzishwa hakukosekani watu wanaopinga siyo wakati wa kurudi nyuma tunatakiwa kusonga mbele,” amesema

 

Previous articleAKAMATWA BAADA YA KUFUNGUA MLANGO WA NDEGE IKIWA ANGANI
Next articleBANDARI KAVU YA KWALA IKO TAYARI KUANZA KAZI, KUPUNGUZA 30% YA MIZIGO INAYOHUDUMIWA NA BANDARI YA DAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here