Home KITAIFA WAKULIMA RUNGWE WALIA NA MAKATO UUZAJI KAHAWA, USHIRIKA WAWASAIDIA KUPATA PEMBEJEO

WAKULIMA RUNGWE WALIA NA MAKATO UUZAJI KAHAWA, USHIRIKA WAWASAIDIA KUPATA PEMBEJEO

 

Na Josea Sinkala, Tukuyu Mbeya.

Wakulima wa zao la Kahawa katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameiomba Serikali kupunguza makato wanayokatwa wakati wa uuzaji zao hilo na kuongeza viwanda ili wakulima kujikomboa kupitia Kilimo.

Pia wakulima hao wameomba Serikali na wadau kufungua viwanda vya kahawa wilayani Rungwe ili kusaidia wakulima kutosafiri umbali mrefu kwenda Mbozi mkoani Songwe kwa ajili kuuza zao hilo.

Wakulima wa Tukuyu wilayani Rungwe wamesema hayo wakati wa mahojiano maalum na Jambo Tv ilipowatembelea wilayani humo na kutaka kujua faida wanazozipata kuendesha shughuli za kilimo wakiwa kwenye Ushirika (Lumbyaa Amcoss).

Wamesema wanapata wanapata faida nyingi kuwa kwenye ushirika ikiwemo kuoata pembejeo za kilimo cha mazao mbalimbali hasa ya kimkakati kwa mkopo.

Emmanuel Mwailonda ni mkulima kutoka Kata ya Mpuguso anasema kuwepo kwake kwenye ushirika kampuni za mbolea zinawasaidia kuwakopesha mbolea ikiwa ni pamoja na mikopo kwenye taasisi za kifedha.

Mwenyekiti wa Lumbyaa Amcoss Willy Mwasyeba anasema umoja huo una wakulima 230 mpaka sasa ambao wamekuwa wkaisaidika katika kuendesha kilimo cha mazao mbalimbali na kuuza mazao yao kwa pamoja.

Amesema uongozi kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Serikali wanashirikiana kuboresha mazingira ya wakulima lakini kero yao kubwa ni umbali wa viwanda viliko (Mbozi Songwe) na kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa Mbolea hivyo kuitaka Serikali kuongeza nguvu kwenye sekta ya kilimo kwa kusogeza mahitaji yao karibu na wakulima na kuwa na pembejeo za kutosha.

Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imekuwa ikiwatembelea wakulima katika maeneo mbalimbali nchini ili kujua maendeleo yake na kutoa ushauri mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia mwenendo wa uuzaji mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mazao na maeneo ambayo tayari yameingia kwenye mfumo huo ambapo Kahawa bado haijafikiwa kwa Wilaya ya Rungwe.

Previous articleCPA.LUDOVICK UTOUH AELEZA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA ELIMU ASEMA MRADI WA HEET UTALETA MAPINDUZI
Next articleALLIANCE IN MOTION GLOBAL WASITISHWA KUFANYA KAZI NJOMBE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here