Home KITAIFA WAKULIMA ILEJE KUJENGEWA UWEZO KUZALISHA PARETO YENYE UBORA

WAKULIMA ILEJE KUJENGEWA UWEZO KUZALISHA PARETO YENYE UBORA

WAKULIMA wa zao la Pareto wilayani Ileje mkoani Songwe wanatarajia kujengewa uwezo kupitia vikundi ili waendelee kuzalisha kwa wingi na kwa viwango zao hilo ambapo wilaya hiyo inashika nafasi ya pili kitaifa kuzalisha pareto yenye ubora unaohitajika na wanunuzi.

Mkuu wa wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi amesema katika kuhakikisha uzalishaji wa pareto yenye viwango inaongezeka wakulima wapewe elimu ya kutosha juu ya aina ya maua wanayotakiwa kuvuna ili kuendeleza ubora wa pareto inayolimwa wilayani humo.

Mhe. Mgomi amesema hayo Juni 26,2023 baada ya baadhi ya wataalamu Idara ya Kilimo, wa halmashauri ya Ileje kutembelea kiwanda Cha kampuni ya Pyrethrum Company Tanzania Ltd (PCT) kilichopo Mafinga mkoani Iringa ambao ni wadau wa kununua Pareto inayolimwa Ileje lengo likiwa ni kujifunza mahitaji ya kampuni hiyo juu ya zao Hilo linalolimwa Ileje kwa mkoa wa Songwe.

Mhe. Mgomi amesema kama wilaya kwa kushirikiana na idara ya kilimo watahakikisha mahitaji ya kampuni ya tani 6000 Kwa mwaka ,Ileje inazalisha Tltani 3000 na hii itatokana na wakulima kupewa elimu ya kulima mashamba makubwa na kulima kitaalamu.

“Tutaendelea kuhamasisha kila mkulima amiliki walau ekari moja, sambamba na kuunda vikundi vya wakulima wa Pareto kwa lengo la kupata nyongeza ya bei mpaka shlingi 4200 pindi watakapovuna awamu ya pili pareto iliyokidhi viwango kulingana na uhitaji wa kampuni”,amesema Mhe.Mgomi.

Afisa kilimo wa wilaya hiyo Hermani Njeje amesema katika kuendelea na kilimo hicho wataunda vikundi vya wakulima vitakavyopewa elimu elekezi ya kuzalisha Pareto yenye ubora unaohitajika hali ambayo itasaidia kuongeza bei ya kununulia kwa kilo.

Njeje amesema kampuni ya PCT Iko tayari kuongeza bei kutoka shilingi 3500 ya sasa mpaka 4200 pindi wakulima watakapozalisha maua ya zao hilo yenye ubora unaohitajika ili kufikia bei hiyo kama wilaya tutahakikisha mawakala wasio kuwa na vigezo wataondolewa Ili kulinda ubora wa pareto yetu.

“Mahitaji ya Pareto ni makubwa kwani sisi kama Ileje tunazalisha tani 1000 kwa mwaka na mahitaji ya kiwanda cha kampuni ya Pyrethrum Company Tanzania Ltd (PCT) ni tani 6000 hivyo tuna kazi kubwa kuhakikisha wakulima wanaongeza uzalishaji yatakayikidhi mahitaji ya kiwanda hicho”,amesema Njeje.

Aidha Njeje alibainisha bei za awali kwa kilo kwa zao hilo ilikuwa ni 1800, 2000, 2500 na Sasa 3500 hivyo bei inatarajia kufika 4200 kupitia kampuni hiyo pindi mkulima atakapozalisha pareto yenye ubora zaidi.

Mwendeshaji mkuu wa kampuni ya Pyrethrum Company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga John Power amesema kiwanda hicho kinashindwa kufanya kazi kwa miezi sita kwa mwaka kutokana na uchache wa zao hilo kwani mahitaji kwa mwaka mzima ni kilo miloni sita.

“Wakulima huzalisha kidogo kulingana na mahitaji ya kiwanda kwani kwa siku tani 18, kwa mwezi tani 375 kwa mwaka tani 6000 zinahitajika , ambapo kwa sasa hupata tani 3000 pekee hivyo kiwanda kusimama Kwa miezi SITA”,amesema John.

Kwa wilaya ya Ileje zao la Pareto hulimwa kwa wingi katika kata ya Ibaba na Itale, ambapo kwa mujibu wa afisa kilimo wa wilaya hiyo Hermani Njeje alisema wanatarajia kuanza uzalishaji kwa kata ya Ngulilo.

Previous articleMAHUJAJI 3000 KUTOKA TANZANIA KWENDA KUHIJI MAKKA .
Next articleREA NA WAKANDARASI WASAINI NYONGEZA YA KAZI KATIKA MIKATABA ILI KUONGEZA KILOMETA MBILI ZA UMEME KWA VIJIJI 4,071

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here