Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwigelo ameandaa mbio za mama wajawazito Wilayani Korogwe, ambazo zimepewa jina la “MAMATHON”,lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa mazoezi na lishe bora kwa Mama na Mtoto.
Akizunguza na waandishi wa habari DC Jokate amesema, mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Jumapili Mei 28,2023 huku dhamira kuu ni kuwafikia Wajawazito 2000 ambao wapo tayari kujifunza kuhusiana na afya ya uzazi, lishe bora na mazoezi kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua.
“Aidha , kupitia mbio hizo tutajikita katika kutoa elimu kwa vitendo pamoja na kugawa vifaa vya kujifungulia kwa Wajawazito”., DC Jokate
” Siku ya mbio hizo tutakuwa na matembezi ya akina Mama wajawazito,mafunzo kutoka kwa wataalamu kuhusu umuhimu wa mazoezi na lishe bora kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua, tutatoa pia Mafunzo juu ya huduma ya M-MAMA.”,DC Jokate