Home KITAIFA WAHUKUMIWA JELA MAISHA KWA KOSA LA UBAKAJI

WAHUKUMIWA JELA MAISHA KWA KOSA LA UBAKAJI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na taasisi zingine za haki jinai katika kudhibiti wimbi la momonyoko wa maadili katika jamii, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali wa kesi za ubakaji, ulawiti na dawa za kulevya, kuwafikisha Mahakamani na kuhukumiwa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuwa mara baada ya ushahidi kutolewa Mahakamani watuhumiwa hao wa ubakaji walihukumiwa ili kuwa funzo kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Maigwa amewataja waliohukumiwa kwa kosa la ubakaji kuwa ni pamoja na Sakaja Iddi Sakaja, (61), mkazi wa wilaya ya Mwanga aliyebaka mtoto wa miaka
7 amehukumiwa kifungo cha Maisha Jela na kazi ngumu, Ernest Kidabiti Nonga, (56), mkazi wa Sanya Juu wilaya ya Siha, alimbaka mtoto wa miaka 7 na amehukumiwa kifungo cha Maisha Jela, Abeid salim Kingazi, (30) mkazi wa Ngarenairobi, wilaya ya Siha alimbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa miaka 17 amehukumiwa kifungo cha 30 kwa kubaka na miaka 30 ya kumpa ujauzito hivyo kuhukumiwa jumla miaka 60 Jela.

Maigwa ametaja wengine kuwa ni Anthony Thadei Mosha, (32) mkazi wa Moshi wilaya ya Moshi alimbaka na kumpa mimba mwanafunzi miaka 16 amehukumiwa kwenda jela kwa kubaka miaka 30 na kumpa mimba mwanafunzi miaka 5 jumla miaka 35 Jela na mwingine Noel Shaha Urasa, (30) mkazi wa Uru Mawela wilaya ya Moshi alimbaka mtoto
wa miaka 9 amehukumiwa Kifungo cha miaka 30 Jela.

Kamanda Maigwa ameeleza kuwa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linaendelea kufanya operesheni mbalimbali na kuimarisha ulinzi na usalama wa Wananchi katika maeneo yote ya mkoa wa Kilimanjaro na hali ya usalama imeendelea kuwa shwari.

Previous articleBENKI YA NBC YAKABIDHI GAWIO LA TSH. BILIONI 20 KWA WANA HISA WAKE, WAJIVUNIA MAFANIKIO
Next articleUMMY ASIMAMISHA WAUGUZI, TUHUMA ZA WATOTO MAPACHA KUCHUNWA NGOZI NA KUNG’OLEWA MACHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here