Home KITAIFA WAHITIMU WATAKIWA KUEPUKANA NA VITENDO VYA UTUMIAJI MADAWA YA KULEVYA

WAHITIMU WATAKIWA KUEPUKANA NA VITENDO VYA UTUMIAJI MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka vijana na wahitimu wa Chuo Cha Sayansi Shirikishi Kilichopo Jijini Mbeya Kuepukana na Vitendo vya Utumiaji wa Madawa ya Kulevya na mapenzi ya Jinsia Moja.

Hayo ameyasema Akiwa kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo hiko Yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Tughimbe ambapo Kutokana na Kukithiri kwa Vitendo hivyo vya mmomonyoko wa maadili amekemea vikali na kuwataka vijana kuwa mstari wa Mbele kupiga vitendo hivyo.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya amesisitiza Wazazi na walezi kutoona aibu Kuzungumza na watoto wao juu ya masuala ya Afya na Maadili

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hiko Dkt Cosmas Chacha ameishukuru Serikali kwa Kutoa kipaombele kwenye sekta ya afya kwa Kuwezesha chuo hiko kutoa elimu Iliyo bora kwa wahitimu wake

Naye Mzazi, Criprian Haule amewataka wahitimu kutokata tamaa Mara baada ya Kuhitimu masomo yao na kuwataka kuwa na subira Wanapokosa Kazi na badala ya yake kujiajiri Pale inapobidi.

Previous article” MAZOEZI YANASAIDIA AFYA KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA”_ DC MVOMERO
Next articleHARRY KANE ASAINI RASMI FC BAYERN MUNCHEN.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here