Home KITAIFA WAHITIMU WA KADA MBALIMBALI ZA AFYA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UAMINIFU

WAHITIMU WA KADA MBALIMBALI ZA AFYA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UAMINIFU

Mkuu wa wilaya ya mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka wahitimu wa kada mbalimbali za afya katika taasisi ya sayansi za afya Mbalizi kufanya kazi Kwa uaminifu pindi watakapopata nafasi za ajira.

Mhe. Malisa ameyasema hayo katika mahafali ya kumi na tisa(19) ya taasisi ya Sayansi za afya Mbalizi yaliofanyika katika hoteli ya Ifisi Community Center (ICC) iliopo Ifisi Halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya.

Mhe. Malisa ambeye ndiye aliekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amesema jambo kubwa katika soko la ajira ni utayari wao wa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na uzalendo kwani Tanzania ni nchi kubwa na inauhitaji mkubwa wa wataalamu wa afya ambapo wao ndo wanahitimu katika mahafali hiyo.

Hata hovyo Mhe. Malisa amesema serikali ya awamu ya sita imetoa fursa lukuki kwa wataalamu wa afya na hivi karibuni zimetoka ajira nyingi hivyo anaamini wahitimu hao wako tayari na wana uzalendo wakutosha na kwamba endapo kama watapata ajira wafanye kazi kwa uaminifu.

Previous articleMALUMBANO YA BANDARI YAMCHEFUA ASKOFU_ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JULAI 22/2023
Next articleUJUMBE KUTOKA KENYA WAJIFUNZA USIMAMIZI SEKTA YA MADINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here