Home KITAIFA WAFUGAJI WATAKIWA KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

WAFUGAJI WATAKIWA KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

 

Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wafugaji jamii ya kimasai kuacha kujichukulia sheria mkononi pale wanapokutana na changamoto mbalimbali hasa za kutuhumiwa kulisha mazao kwenye mashamba ya wakulima.

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi Mkoa huo kamishna msaidizi wa Polisi Alex Mkama, katika kijiji cha Maharaka kata ya Doma Wilaya Mvomero alipofanya kikao na baadhi ya wafugaji katika kijiji hicho na kuwataka wafugaji hao kuwa watulivu katika kipindi hiki cha kesi yao ya Kujeruhiwa kwa ng’ombe 13 walipopelekwa mtoni kwaajili ya kunywa maji.

” Mnatakiwa kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho kesi yenu ya kujeruhiwa kwa ng’ombe zenu 13 inaendelea ili mpate haki zenu maana hiki kilichotendeka ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi yetu, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria” alisema kamanda Mkama.

Aidha Mkama aliwataka wafugaji hao kuishi kwa amani na kuepuka migogoro inayoepukika kati yao na wakulima kwani migogoro hiyo inaondoa amani na utulivu mara inapotokea katika maeneo yao.

Previous articleSERIKALI YASEMA ITAENDELEA KUWAUNGA MKONO WADAU WA SEKTA BINAFSI
Next articleKUCHELEWESHWA KWA FEDHA YA KUJIKIMU KWAPUNGUZA ARI YA UTENDAJIKAZI HALMASHAURI YA WILAYA MOROGORO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here