Mkaguzi msaidizi wa Polisi Stephen Mwita amewataka wafanyakazi wa machinjio ya Kitete kata ya Ruaha Mikumi Mkoa wa Morogoro kuzingatia usafi katika maeneo hayo pamoja na vifaa wanavyotumia kuchinjia na kuandaa nyama kwaajili ya kumfikishia mlaji katika ubora.
Akitoa elimu katika machinjia hayo Mwita amesema usafi usipozingatiwa katika maeneo ya machinjio kunaweza kusababisha milipuko ya magojwa kwa walaji wa nyama hivyo kama polisi kunasababu ya kukumbushana kuhusu usafi kwa kutoa elimu.
Pia Mkaguzi msaidizi huyo wa polisi Mwita ametoa elimu ya programu ya miradi ya Polisi ambayo inatambulika kwa usalama wetu kwanza na mazizi salama kwani kunabaadhi yao wanamifugo yao.
Kwa upande mwingine katika machinjio ya Wilaya ya Gairo, Sajenti wa Polisi Dasmas John na Coplo Jacob Arbogast wa kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo Wilaya ya Gairo, wamewaasa wafanyakazi wa machinjio katika Wilaya hiyo kuacha kupokea mifugo ya wizi na badala yake watoe taarifa kwa wahalifu wanaojihusisha na wizi huo wa mifugo.