Home KITAIFA WAFANYABISHARA WAPIGWA MSASA JUU YA UTUNZAJI FEDHA

WAFANYABISHARA WAPIGWA MSASA JUU YA UTUNZAJI FEDHA

 

Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kata ya Kiroka Insp.Dhikiri Pori, amewatembelea wafanyabiashara wadogo katika soko la Kiroka Mkuyuni Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa lengo la kuwapa elimu ya namna ya utunzaji wa fedha.

Akiongea na wafanyabiashara hao Insp.Pori amesema ni wakati sasa wa kuwapatia wafanyabiashara wadogo elimu pamoja na mbinu za kutunza fedha ili kuweza kukuza biashara pamoja na kufanya biashara katika mazingira safi na salama.

Pia amesisitiza kuwa wafanywbiashara hao kuacha kufanya biashara kwa mazoea hivyo wametakiwa kubadilika kutokana na ulimwengu unavyoenda .

Aidha kwa upande mwingine Insp. Pori amewakumbusha wakina mama wafanyabiashara kuwa biashara isiwe kigezo cha kuacha kuhudumia familia pamoja na kuwa karibu na watoto ili kupunguza vitendo vya kikatili kwa watoto.

Previous articleBUNGE LATOA MSIMAMO SAKATA LA BANDARI…YANGA YAKAA MAHALI PAKE _ MAGAZETINI LEO JUMATANO AGOSTI 30/2023
Next articleZAHANATI ZA KATA YA MKANGE HAZINA MANESI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here