Home KITAIFA WAFANYABIASHARA WA NCHI ZA ZAMBIA, DR CONGO, BURUNDI WAIKUBALI BANDARI YA KAREMA,...

WAFANYABIASHARA WA NCHI ZA ZAMBIA, DR CONGO, BURUNDI WAIKUBALI BANDARI YA KAREMA, WAWASILISHA CHANGAMOTO YA BARABARA KUELEKEA BANDARINI

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula akitoa taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Karema kwa waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo Juni 03, 2023

 

 

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula akitoa taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Karema kwa waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo Juni 03, 2023

 

Mwonekano wa miundombinu mbalimbali katika bandari ya Karema

Na Mwandishi Wetu, Katavi

Katika kuhakikisha kwamba bandari ya kimkakati ya Karema iliyopo wilayani Tanganyika mkoani Katavi inafanya kazi vizuri zaidi na kuongeza mapato, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya vikao na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kutoka nchi za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi kwa lengo la kuendeleza ushirikiano wa kibiashara kwa kuitumia bandari hii ombi ambalo lilikubaliwa likiambatana na changamoto walizowasilisha wadau hao.

Changamoto kubwa iliyowasilishwa na wadau pamoja na watumiaji wa bandari ambao wanapitisha mizigo yao katika bandari hiyo hiyo ni ubovu wa barabara ya kuelekea katika bandari hiyo.

Hayo yamesemwa Juni 03, 2023 na Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema mbali na changamoto hiyo ya barabara lakini pia kukosekana kwa miundombinu ya reli katika bandari hiyo ni changamoto nyingine.

Mbali na changamoto hizo, Mabula amesema, bandari hiyo imeweza kuhudumia tani 4,500 ya shehena ya mzigo mbalimbali na abiria 2970 hadi kufikia mwezi Mei, mwaka huu.

Mabula ameongeza kuwa, serikali imeshaanza kutekeleza mikakati ya kuongeza uwezo wa kutoa huduma bandari za ziwa Tanganyika ikiwemo Karema kwa kuanza ujenzi wa meli mbili kubwa za kisasa na kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya kuelekea katika bandari ya Karema.

“Tuna ahadi ya serikali ya kujenga meli mbili kubwa, moja yenye uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 3,000 na nyingine yenye uwezo kuchukua abiria 400 na tani 600 za mizigo, tayari ujenzi wa meli hizi umeshaanza” alisema Mabula na kuongeza

“Barabara ya kuelekea katika bandari Karema imetangazwa katika gazeti la serikali na taratibu za kumpata mkandarsi zinaendelea baada kuwa muda wa zabuni kukamilika mwisho wa Mei, mwaka huu”

Aidha, Mabula ametumia fursa hiyo kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza katika bandari ya Karema kupitia fursa mbalimbali zinazotokana na bandari hiyo ikiwemo kuwekeza katika vyombo vya usafiri kama vile meli na boti.

Kwa upande wake nahodha wa boti inayofanya shughuli za usafiri na usafirishaji kati ya nchi ya Tanzania na Jamhuri ya Muungano wa , Amos Kapena amesema kuwa, kufuatia maboresho yaliyofanywa katika bandari hiyo yamepunguza gharama na hasara kwa mteja na wamiliki wa vyombo.

Kapena amebainisha kuwa, hasara na gharama hizo zilitokana na kushindwa kwa meli au boti kupakuliwa bandarini na hivyo kutumia mitumbwi kupakua mizigo na kuufikisha katika bandari.

Nahodha Almas Kapena akielezea kuhusu huduma zinazotolewa sasa hususan za kupakia na kupakua mizigo namna zilizovyoboreshwa katika bandari ya Karema

Naye mmoja wa wananchi wa Karema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanganyika, Joseph Edward amesema ujio wa bandari ya Karema umeleta manufaa lukuki kwa wakazi wa Karema, wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi na Taifa kwa ujumla.

Joseph ameyataja manufaa hayo ni pamoja na furza za ajira wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi, kukua kwa biashara kufuatia ongezeko kubwa la wageni na watumiaji wa bandari hiyo.

Mwananchi na mkazi wa Karema, Joseph Edward akiongelea na wananchi walivyonufaika na uwepo wa bandari hiyo

Bandari ya Karema ipo kilomita 123 kutoka Mpanda ambapo ujenzi wake ulianza mwaka 2019 kwa gharama ya shilingi Bilioni 47.9 ambapo sasa inatajwa na wafanyabiashara kama mkombozi wa uchumi wao kwa kusafirisha bidhaa zao kutoka Tanzania kwenda nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Burundi bila wasiwasi.

Previous articleMKOA WA KAGERA NI MKOA MASKINI ZAIDI NCHINI” ZITTO KABWE 
Next articleUWAWATA WALAANI VITENDO VINAVYOFANYWA NA KAMCHAPE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here