Kata nne ambazo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto ya maji katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro zimepatiwa visima vinne vya maji kutoka kwa wafadhili kutoka nchini Uswisi lengo likiwa ni kuitatua changamoto hiyo.
Wananchi wa kata hizo nne za Euga Chilombora,Uponera na Kichangani wamesema wamekuwa wakikubwa na adha hiyo ya maji kwa mda mrefu hivyo visima hiyo vitaenda kuondoa adha hiyo.
Mwakilishi wa wafadhili hao Rubab Jawad Aziz amesema, hatua hiyo imekuja baada ya kuona changamoto ya maji imekuwa kubwa katika Wilaya hiyo licha ya serikali kupambana kuitatua mara zote.
Naye Mbunge wa Jimbo hilo la Ulanga Mhe .Salim Alaudin Hasham amesema ,changamoto ya maji katika jimbo hilo ni kubwa hivyo hawezi kuiachia Serikali pekee bali ataendelea kutafuta wadau wengi kwa lengo la kuhakikisha changamoto hiyo inapungua kama sio kuisha kabisa.