Home KITAIFA WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI 

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI 

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza ( MPC ), Edwin Soko amewaomba waandishi wa habari wafate sheria na kanuni za uandishi wa habari.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza katika Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, amesema waandishi wa habari wanakumbana na changamoto katika kufanya kazi kama swala la kiusalama.

Amesema mkoa wa Mwanza umefanikiwa kupata mahusiano mazuri na jeshi la polisi kwa kuitisha midaharo na kujadili kuhusiana na changamoto wanazopitia.

Akizungumza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, Wilboard Mutafungwa amesema Jeshi la polisi la mkoa linahaidi kulinda usalama na haki za waandishi wa habari wakati wa kufanya kazi zao.

 

Aidha amesema waandishi wa habari wahakikikishe wanapata vitambulisho vya kazi ili kutofautisha kati ya waandishi wa habari na raia wa kawaida ili kulinda usalama wao.

 

Akiongezea kusema waandishi wa habari wanapaswa kuwa weledi kama sehemu wanayoenda kuchukua habaru kuna utepe mwekundu wa polisi inabidi waonane na uongozi kwanza.

 

”Nipende kutoa hongera kwa kuweza kuwa na umoja wa chama cha uandishi wa habari Mwanza niwaombe midaharo iweze kuongezeka lakini pia niwaombe kuweza kuwaombea na kuwakumbuka waandishi wenzenu waliofariki dunia na waliopata majeraha katika majukumu ya kutekeleza kazi ya uandishi wa habari”_ Amesema Mutafungwa

Previous articleWANAFUNZI 593 WANUFAIKA NA SAMIA SCHOLARSHIP
Next articleSERIKALI KUSHIRIKISHA WANANCHI KUHUSU KUONDOLEWA KWA KIJIJI CHA NGARESERO KWENYE PORI TENGEFU LA POLOLET, NGORONGORO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here