Home KITAIFA VYAMA VYA USHIRIKA VYASHAURIWA KUPITIA HESABU ZA VYAMA VYAO MARA KWA MARA.

VYAMA VYA USHIRIKA VYASHAURIWA KUPITIA HESABU ZA VYAMA VYAO MARA KWA MARA.

 

Kamati ya ukaguzi Tume ya Maendeleo ya Ushirika imefanya ziara mkoani Mwanza na kukagua Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza NCU ( 1984 ) kwa kukutana na Bodi ya chama hicho kisha kupata taarifa fupi kuhusu shughuli za NCU 1984, na kugundua changamoto mbalimbali na kutoa ushauri wa kuhakikisha mali zote ambazo ni za chama hicho ziweze kurudishwa.

 

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Maendeleo ya Ushirika Evance Assenga Mkoani Mwanza katika ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua vyama vya ushirika Jijini Mwanza.

Aidha Assenga amewataka wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Fsa kilichopo kata ya Mkolani Jijini Mwanza kuhakikisha kinakaguliwa katika hesabu zake na mkaguzi wa nje ikiwa sambamba na kupitia ripoti zote za mkaguzi wa ndani,

 

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Tume hiyo,amevishauri Vyama vya Ushirika vya Wavuvi vilivyopo katika Mwalo wa Kimataifa wa samaki Jijini humo mambo mbalimbali kwa kuhakikisha wanandaa hesabu za chama hicho pamoja na kutoa taarifa za masoko na kufanya uwekezaji ili waweze kunufaika.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika NCU Benjamin Makomangwa ameiomba Serikali iweze kukipatia sapoti chama hicho kutokana na kushindwa kujiendesha kwa muda mrefu hivi sasa kwa kukosa raslimali fedha za ukarabati wa baadhi ya majengo ikiwemo Viwanda ambavyo vinamilikiwa na ushirika huo.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Mwaloni Saccos kilichopo katika eneo la mwalo huo, Erasto Lameck amesema, wanakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo kukosa maeneo ya uvuvi hasa katika fukwe za Ziwa Victoria ambazo zimeuzwa kwa minajili ya shughuli za matumizi mengine ya kibinadamu tofauti na kutumika katika masuala ya uvuvi.

” Hivyo tunaiomba Serikali iweze kutenga maeneo ya sahihi kwa ajili ya wavuvi kwasasa ukiangalia katika fukwe zote zimepimwa nimewekwa bikoni sijui wavuvi wataenda wapi na chakula cha samaki ndio matarajio ya watu, Erasto Lameck, Mkiti Mwaloni Saccos Mwanza.

Previous articleUPINZANI WAPINGA BAJETI YA SH. MIL. 220.6 MANUNUZI MAVAZI YA RAIS MUSEVINI
Next articleWAPENI WANANCHI WANGU PIKIPIKI ZAO NA MUWAPE ELIMU ILI WASIVUNJE SHERIA – SALIM ALMAS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here