Home KITAIFA “VYAMA VYA SIASA TUNAKUPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA MAENDELEO NA UMOJA”_KINANA

“VYAMA VYA SIASA TUNAKUPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA MAENDELEO NA UMOJA”_KINANA

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi( CCM)Abdulrahman Kinana amesema vyama vya siasa nchini vinampongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoleta maendeleo, maridhiano na kuimarisha umoja katika Taifa.

Akizungumza leo wakati akitoa salamu kwa niaba ya vyama vya siasa kwenye Tamasha la Kizimkazi visiwani Zanzibar, Ndugu Kinana alisema anajivunia uongozi wake.

“Nina hakika mimi binafsi nimekua na mazungumzo mara kadhaa na viongozi wa vyama vya siasa, tulikaa siku tatu na vyama vyote katika baraza la vyama vya siasa, kila chama kiliposimama kilikupongeza kwa kadri unavyoongoza nchi vizuri.

“Kwa namna ulivyoleta maridhiano , kwa namna ulivyoimarisha umoja wa taifa letu, Amesema Kinana.

Kuhusu Tamasha la Kizimkazi Kinana amesema limefanikiwa kuweka misingi mizuri ya kujenga muungano wa nchi yetu na kwamba katika siku zijazo litakuwa la kimataifa.

“Shughuli hii ya Kizimkazi ambayo ni shughuli ya sanaa, utamaduni , michezo, furaha, burudani na bashasha.Shughuli hii inafanyika Kizimkazi lakini shughuli hii ni ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla.

“Kwa namna nilivyoona shughuli hii sio tu ya Zanzibar lakini ni shughuli iliyoweka misingi mizuri ya kujenga muungano wa nchi yetu, ” amesema Kinana.

Amefafanua kwenye tamasha hilo wako watanzania wengi kutoka nje ya Zanzibar na anahakika watakuwa wengi zaidi siku zijazo kuja Kizimkazi sio tu kuona lakini kushiriki.

Previous articleJELA MAISHA KWA KUMUINGILIA MTOTO (9) KINYUME NA MAUMBILE
Next articleKIKWETE AWATAKA WADAU KUTIMIZA AHADI ZAO ZA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA SEKTA YA ELIMU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here