Home KITAIFA VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA AMANI KWA MANUFAA YA WANANCHI

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA AMANI KWA MANUFAA YA WANANCHI

 

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha wasimamia haki na kuienzi na kusimamia amani kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

 

“Niwasihi sana ninyi viongozi wetu wa dini kutukumbusha mara kwa mara sisi, waumini na watu wote kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani na kuiombea nchi yetu na viongozi wake” alisema Majaliwa.

 

Majaliwa alisema hayo Jana katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa  Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa  Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Imani wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

kupitia harambee hiyo ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria-Mwanza Kanisa hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 119,563,000 zikiwemo fedha taslimu, ahadi na vifaa.

 

Kupitia hotuba yake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa dini nchini kutochoka kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi  halali.

 

” Katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii yeru, vitendo viouvu na mambo yasiyopendeza mwenyezi Mungu yanazidi kuongezeka mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikia lakini sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana eti ya kawaida” alisema majialiwa kupitia hotuba yake.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia sana na kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo na kuifanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.

 

Amesema, anaamini kwa dhati kuwa viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuoongozwa vizuri.

” Naendelea kuwaomba kwa niaba ya serikali, viongozi wa dini zetu zote tusaidiane kukea taifa letu kimaadili na tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu kwanza wao ndiyo wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka lakini pia wao ni taifa la leo na viongozi wa kesho” alisema

 

Kupitia hotuba yake hiyo, Majaliwa alisisitizia pia suala la elimu na kueleza kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote na kutaka viongozi wa dini kusaidia kuzungumza na wazazi na kuwaslimisha kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto.

 

Amelipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria -Mwanza na waumini kwa ujumla kwa kujitoa kwa hali na mali kwa  kufanya kazi ya Mungu kwa kuhakikisha jengo linakamilikia hasa ikizingatiwa fedha zote ni michango ya waumini na kubainisha kuwa, kitendo kilichofanyika ni chema na kinaleta baraka zote.

Awali Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle alisema ujenzi wa shule ya kanisa hilo unakadiriwa kuwa na gharama ya Shilingi 2,350,000,000 ambapo amesema mpaka sasa kiasi cha 430,000,000 kimetumika kujenga boma la madarasa kumi na boma la jingo la utawala.

 

Katika harambee hiyo ya ujenzi wa shule Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alichangia shilingi milioni 5 ili kutumika kukamilisha kazi ya ujenzi wa shule huku Dkt Mabula kuchangia milioni 2 katika ujenzi huo

 

Previous articleMISHAHARA YA APRILI ILIPWE MAPEMA “_ RAIS MWINYI
Next articleTANROADS KUPITIA WAKANDARASI WAZAWA, YAKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI RUDEWA-KILOSA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here