Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Mbeya Vijijini kushirikiana na viongozi wa Serikali ili kulinda vyanzo vya maji.
Mhe. Malisa ameyasema hayo kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Jimbo la mbeya Vijijini uliofanyika jana Juni 30/2023 katika ukumbi wa Lehner uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi.
Mhe. Malisa amesema mkoa wa mbeya unamilima mingi ambayo ni kikwazo cha upatikanaji wa maji na hata kama yakipatikana chini ni gharama kubwa kuyafikisha kwa wananchi, hivyo vyanzo vichache vilivyopo viwekewe mkakati wa makusudi wa kuvilinda.
Hata hivyo Mhe. Beno Malisa amemsema viongozi wa chama ndio wanaoishi na wananchi kwa ukaribu na ndio wanaojua kwa ukaribu zaidi watu wanaoharibu vyanzo hivyo vya maji na kwamba wanauwezo wakutoa taariba pindi wanapoona kuna uharibifu.
Mhe. Malisa amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa katika sekta ya maji hivyo viongozi wanakila sababu ya kulinda vyanzo na miundombinu ili maji yawafikie wananchi kwa uhakika zaidi.