Home KITAIFA VIJANA WAKUMBUSHWA KUWAKUMBUKA WAZEE ILI KUVUNA BARAKA

VIJANA WAKUMBUSHWA KUWAKUMBUKA WAZEE ILI KUVUNA BARAKA

 

 

Jamii nchini imetakiwa kuendelea kuwakumbuka watu wenye uhitaji kwa kutoa msaada wa vitu mbali mbali ili kusaidiana na kutatua changamoto ambazo watu wakiwemo wazee kwenye jamii wameendelea kukabiliana nazo.

Wito huo umetolewa na baadhi ya vijana wazawa wa kijiji cha Igola kilichopo mjini Njombe akiwemo Feliki Mwalongo na Basilisa Mwalongo walipokwenda kumtembelea Bibi Rainfrida Mgaya ambaye ni mkazi wa kijiji hicho mwenye umri wa zaidi ya miaka 100.

“Nitoe wito kwa vijana wenzangu kwamba warudi nyumbani wawasaidie wazazi kwasababu tunakosa baraka wakati mwingine kwasababu ya umimi”alisema Feliki Mwalongo

Stephano Msemwa ni mwenyekiti wa kundi la Njilikwa Fans (Marafiki wa Njilikwa) amesema kupitia wananchama waliopo kwenye kundi hilo wamefanikiwa kutoa msaada wa vitu mbalibali ikiwemo godoro ili kumsaidia bibi huyo anapopumzika.

“Siku ya leo kwa huyu bibi tumekuja kutoa msaada wa godoro,chumvi,sabuni lakini pia hata tochi kwasababu vitu kama hivi tunajua bibi anauhitaji mkubwa”alisema Msemwa

Bibi Rainfrida Mgaya ameshukuru vijana hao kwa kumsaidia kwa kuwa amekuwa akiendelea kuishi kwa kupata msaada kutoka kwa watu mbali mbali kutokana na umri wake.

“Ninashukuru sana na Mungu awabariki muendelee kunilinda”alisema Bibi Rainfrida Mgaya kwa lugha ya kibena

Previous articleBUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI 3 MWAKA 2023
Next articleWATATU WATIWA HATIANI KWA KOSA LA KUUA BILA KUKUSUDIA KISA WIVU WA MAPENZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here