Home KITAIFA VIJANA VIONGOZI 50 WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WAMEJILIPIA MAFUNZO YA UONGOZI...

VIJANA VIONGOZI 50 WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WAMEJILIPIA MAFUNZO YA UONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIAS NYERERE KIBAHA

Na Scolastica Msewa, Kibaha

VIJANA wanaochipukia katika nafasi mbalimbali za uongozi kutoka katika vyama mbalimbali vya kisasa nchi 50 wa Tanzania na Afrika Kusini wamejiunga na Mafunzo ya kujengewa uwezo wa uongozi katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere ya Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani kwa wiki Moja.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Profesa Mercelina Chijoriga wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati akipokea vijana hao zaidi ya 50 kutoka Tanzania na Nchini Afrika ya kusini waliofika kwa ajili ya mafunzo hayo kwa uongozi ya vijana.

Alisema ni wajibu wa vijana wa kitanzania wanaochipukia katika nafasi za uongozi kufika katika shule hiyo na kupatiwa mafunzo sahihi yatakayo wasaidia kuongoza Kwa kuzingatia maadili ili kuwa viongozi Bora wa baadae wenye tija katika taifa.

“Inasikitisha kuona vijana wa kitanzania kushindwa kuchukulia umuhimu wa mafunzo tunatoka hapa shuleni nasisitiza wafike na tuwape mbinu mbalimbali za uongozi wataona faida zake..sisi tumetoa kozi za masuala ya kisaisa zaidi ya 10 na tutaendelea kutoa kadri ya mahitaji” alisema Chijoriga

Akizungumza mafunzo ya vijana hao alisema mafunzo hayo yamewakutanisha vijana Kutoka sekta binafsi na sekta ya umma na kwamba ni mahususi Kwa vijana wanaoibukia katika uongozi lengo likiwa ni kuwapa mbinu mbalimbali za kiuongozi ikiwemo kufundishwa misingi na kanuni za uongozi Bora

“Mafunzo haya ni ya siku sita na yatahusisha vijana wengi kutoka hapa nchi lakini 13 kati Yao wanatoka nchini Afrika kusini watajifunza uzalendo na kupenda utaifa, historia wa bara la afrikana suala jingine ni kuhusu masuala ya kiuchumi maana tumepata uhuru wa bendera Ila kwenye uchumi bado”alisema.

Hatahivyo amewataka vijana viongozi kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo ya uongozi yanakayo wajenga kuwa wazalendo, kuzingatia utawala Bora na waadilifu katika utendaji wao wa uongozi.

Aidha alisema mafunzo hayo ambayo yameanza yatafunguliwa rasimi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa. Kitila Mkumbo.

Naye mnufaika wa mafunzo hayo Khadija ISSA Juma, Mwenyekiti wa jukwaa la wazalendo huru alisema mafunzo hayo yatawasaidia kujua umuhimu wa kuwa kiuongozi mzalendo na mwenye maadili.

Previous articleWAZEE WAKUMBUSHWA JUKUMU LA KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI NCHINI
Next articleUWT YAWATEMBELEA WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HOSPITALI YA RUFAA MANYARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here