Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela ametoa wito kwa vijana kuzielewa vizuri kazi na miradi inayotekelezwa na serikali ili waweze kuisemea vizuri machoni kwa watu.
Ametoa wito huo wilayani Makete wakati wa uzinduzi wa wimbo wa nasimama na mama ulioimbwa na msaniii Rauford Chaula (Mackford) wa kutoka kwenye wilaya hiyo ambapo amebainisha kuwa wimbo huo umeeleza mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Samia na kubainisha kuwa vijana wanapaswa kuwa na uelewa zaidi juu ya miradi ili kuwa na jambo la kusema.
“Rais mwenyewe hawezi kujisemea kwa hiyo vijana lazima muelewe kazi zilizofanywa na lazima tumsemee,kwanza amani imetawala na nchi imetulia na hiyo ndio sifa pekee kubwa tuliyo nayo,kwa hiyo vijana na viongozi wote tujue na tujifunze kazi alizofanya mpendwa wetu Dkt Samia Suluhu Hassan “amesema Scolastika Kevela
Awali akisoma risala wakati wa uzinduzi wa wa wimbo huo wa nasimama na mama bwana Rabson Mahenge ambaye ni msimamizi wa msanii amesema wimbo huo utakwenda na kampeni ya nchi nzima yenye jina la Nasimama na mama huku lengo ikiwa ni kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan.