Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa ametoa rai kwa Vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo ya JKT,kuzitumia stadi za kazi na maisha walizozipata kujiajiri na kujitegemea.
Waziri Bashungwa amesema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
“Wizara kupitia JKT imeendelea kuwapatia Vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, stadi za kazi,kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa, katika mwaka wa fedha 2022/2023, mafunzo yamefanyika kwenye kambi mbalimbali za Jeshi kupitia Oparesheni ya Jenerali Venance Mabeyo,Vijana 24,458 kwa mujibu wa sheria wamepatiwa mafunzo, kati yao 17,942 wa kiume na 6,516 wa kike”. Innocent Bashungwa
“Kwa upande mwingine,Bashungwa amesema Vijana 11,358 wa kujitolea wamepatiwa mafunzo,kati yao 7,483 ni wa kiume na 3,875 ni wa kike,dhumuni la mafunzo hayo ni kuwawezesha Vijana kuwa raia wema ,wazelendo na wenye uwezo wa kujitegemea na kulilinda Taifa.” Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ,Innocent Bashungwa