Home KITAIFA VIJANA 600 KUSHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA KESHO DODOMA.

VIJANA 600 KUSHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA KESHO DODOMA.

 

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana Agosti 12, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na wadau imeandaa kongamano la kitaifa la vijana litakalofanyika kesho jijini Dodoma.

Kongamano hilo litashirikisha vijana 600 ambapo pamoja na mambo mengine vijana watajadili ustawi na maendeleo yao.

Hayo yemeelezwa Agosti 10, 2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu, wakati akizungumza na waandishi wa habari

Amesema siku ya kilele vijana watashiriki katika shughuli za maonesho na bonanza katika viwanja vya chang’ombe Dodoma na watapatiwa huduma za upimaji wa afya kwa hiari, ushauri nasihi, elimu ya afya ya uzazi pamoja na kujitolea kuchangia damu salama ili kuwasaidia wahitaji katika hospitali nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘Kuelekea 2030: Vijana na Ujuzi wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu’ inayokumbusha jumuiya za kimataifa suala la kulinda na kuhifadhi mazingira.

Previous articleWIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAFUNGUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA
Next articleWAPOTOSHAJI BANDARI WAANGUKIA PUA…DABI YA KARIAKOO KUPIGWA TANGA_ MAGAZETINI LEO IJUMAA AGOSTI 11/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here