Home KITAIFA UWT YAWATEMBELEA WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HOSPITALI YA RUFAA MANYARA

UWT YAWATEMBELEA WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HOSPITALI YA RUFAA MANYARA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya UWT na viongozi wa mikoa ya Manyara na Arusha Desemba 05, 2023  wamefika kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na mawe kutoka Mlima Hanang, Katesh mkoani Manyara.

Chatanda ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na serikali katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara na sisi kama Umoja wa wanawake Tanzania  UWT tumeona tuje tuwaone wananchi wetu wa Hanang kwa kuja kuwafariji kwa kidogo ambacho kama UWT tumekipata  na tutaendelea kuleta misaada mbalimbali kwenu ili iweze kuwasaidia .

Previous articleVIJANA VIONGOZI 50 WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WAMEJILIPIA MAFUNZO YA UONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIAS NYERERE KIBAHA
Next articleUWT YATOA MSAADA KWA WANANCHI WA HANANG

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here