Home KITAIFA UWT YATOA MSAADA KWA WANANCHI WA HANANG

UWT YATOA MSAADA KWA WANANCHI WA HANANG

UWT YATOA MSAADA KWA WANANCHI WA HANAN

Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda  amekabidhi msaada  wa vitu mbalimbali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera ,Bunge na Uratibu ) Mhe Jenista Mhagama Desemba 05, 2023 walipowatembelea wakiwa na wajumbe wa kamati ya maafa ya UWT na viongozi wa mikoa ya Manyara na Arusha  katika kuwapa pole walioathirika na Mafuriko hayo

Chatanda ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kwa hakika huu msiba mzito ambao umeshtua Taifa na kila mtu  na sisi kama umoja wa wanawake Tanzania tumejikusanya kwa umoja wetu kuleta msaada huu ambao utasaidia kwa wananchi wetu wa Hanang.

“Sisi tulikuwa Rufiji kwenye Tamasha la Kumuenzi Bibititi Mohamed, lakini tukapata taarifa hii na baadae tukaona kwenye  vyombo mbalimbali vya habari  tukasema kweli hali ni mbaya, ndivyo  tukaketi na kamati yangu ya utekelezaji tukaamua tuje na hiki  kidogo kwa ajili ya kurejesha tabasamu  kwa watu ambao wamepata shida hii “Amesema Chatanda.

Previous articleUWT YAWATEMBELEA WAGONJWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HOSPITALI YA RUFAA MANYARA
Next articleUWT YAREJESHA TABASAMU KWA WANANCHI WA HANANG, YATOA MSAADA WA MABLANKETI, MASHUKA NA MAHITAJI MENGINE MUHIMU, YAUNDA KAMATI MAALUM YA MAAFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here