Home KITAIFA UWT YAREJESHA TABASAMU KWA WANANCHI WA HANANG, YATOA MSAADA WA MABLANKETI, MASHUKA...

UWT YAREJESHA TABASAMU KWA WANANCHI WA HANANG, YATOA MSAADA WA MABLANKETI, MASHUKA NA MAHITAJI MENGINE MUHIMU, YAUNDA KAMATI MAALUM YA MAAFA

Na Mwandishiwetu

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mama Mary Chatanda ameongoza wanawake wa CCM Tanzania kutoa salamu za pole kwa wakazi wa Hanang mkoani Manyara kutokana na madhara waliyoyapata kwenye mafuriko.

Akizungumza na wakazi wa Hanang Mama Chatanda amesema kwa hakika huo ni msiba mzito ambao umeshtua Taifa na kila mtu .

“Sisi tulikuwa Rufiji kwenye Tamasha la Kumuenzi Bibi Titi Mohamed, lakini tukapata taarifa hii na baadae tukaona kwenye vyombo mbali mbali vya habari tukasema kweli hali ni mbaya ndivyo tukaketi na kamati yangu ya utekelezaji tukaamua tuje na hiki kidogo kwa ajili ya kurejesha tabasamu kwa watu ambao wamepata shida hii “Amesema Chatanda.

Mama Chatanda amesema kupitia wadau na michango iliyotolewa na wanawake wa UWT kutoka kila pembe ya nchi imeweza kufanikisha kupatikana kwa kidogo hiki.

Mama Chatanda alitaja UWT imeweza imeweka kutoa magodoro 300, khanga 1000, mablanketi ,mashuka ya kimasai ,sabuni na vingine vingi.

Amesema pia michango bado inaendelea na UWT imeunda kamati ya maafa ambayo inaratibu michango yote na wametoa agizo kwa wabunge wanawake kutoa michango ya hali na mali na kusema kuwa mpaka sasa wabunge wamechanga shilingi milioni 10.

Aidha Mama Chatanda alipata fursa ya kutembelea maeneo walipohifadhiwa wahanga wa mafuriko hayo na Hospital ya Kateshi na kuwapa pole majeruhi wote.

Previous articleUWT YATOA MSAADA KWA WANANCHI WA HANANG
Next articleNILIKUWA NATOA HARUFU KALI HADI MUME WANGU KANISUSA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here