NA DENIS SINKONDE, SONGWE
Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania CCM mkoa wa Songwe imetembelea shule ya sekondari Vwawa na kutoa vitu mbalimbali Kwa wanafunzi baada ya bweni la wanafunzi kuungua Kwa moto hivi karibuni.
Jumuiya hiyo imeongozwa na mwenyekiti wake Emelia Mwakyoma Aprili 20,2023.
Mwakyoma kwaniaba ya jumuiya amekabidhi mashuka, Sabuni na nguo za ndani Kwa wanafunzi hao lengo likiwa ni kuwafariji baada ya vitu vyao kuteketea Kwa moto.
Baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mwakyoma amewasihi wadau wengine kuendelea kujitolea kutoa msaada kuwapa wanafunzi Ili wasiwe na hofu ya mahitaji katika kipindi ambacho wanafunzi hao ambao wapo kidato Cha sita wataanza mitihani ya kitaifa ya kuhitimu
Mwakyoma ameongeza Kwa kuawaasa wanafunzi hao waendelee kuamini kuwa watafauru mitihani yao kwani Mungu yu pamoja na watarajie walichokisoma na kukielewa ndicho kinaenda kutokea kwenye mitihani yao.