Home KITAIFA UWINDAJI WA KITALII WANUFAISHA NCHI, BIL.9.6 ZATOLEWA KWA HALMASHAURI NA VIJIJI PEMBEZONI...

UWINDAJI WA KITALII WANUFAISHA NCHI, BIL.9.6 ZATOLEWA KWA HALMASHAURI NA VIJIJI PEMBEZONI MWA MAPORI AKIBA NA TENGEFU

 

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi Nyanda amesema shughuli za uwindaji wa kitalii zinazofanywa katika mapori ya akiba na mapori tengefu yanayosimamiwa na TAWA nchini , zina manufaa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja hususani wale waishio pembezoni mwa mapori ya akiba na mapori tengefu .

Kamishna Kabula ameyasema hayo jana katika ofisi za pori la akiba kizigo lililopo Wilaya ya Manyoni mkoani Singida akiongea na watumishi wa pori hilo katika ziara yake ya kikazi kanda ya kati.

Kamishna Mabula amesema serikali kupitia TAWA imetoa jumla ya shilingi billioni 9.6 Kwa Halmashauri na Vijiji wanufaika wanaoishi pembezoni mwa mapori ya akiba na mapori tengefu nchini ikiwa ni fedha zitokanazo na asilimia 25 ya ada ya wanyamapori waliowindwa pamoja na utalii wa picha katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 mpaka Desemba 2022.

Katika ziara hiyo, Kamishna Mabula,amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji safi, nyumba za watumishi na ofisi pamoja na kukutana na kuzungumza na viongozi wa kanda ya kati TAWA pamoja na kuwapongeza juu ya utendaji kazi wao.

Pia Kamishna Mabula amewaagiza viongozi na watumishi wa kanda ya kati kuhakikisha vitalu vyote vya uwindaji wa kitalii katika pori la akiba Kizigo vinapata wawekezaji.

Previous articleMAPYA KIFO CHA MWANAFUNZI WA UDOM FAMILIA YAFUNGUKA YADAI MWILI ULIVIKWA NGUO ZA KIUME_ MAGAZETINI LEO ALHAMISI MEI 11/2023
Next articleUVCCM TAIFA WAIOMBA SERIKALI KUVIPANDISHA HADHI VYUO VYA KILIMO NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here