Home SIASA “UWEKEZAJI WA DP WORLD NI HATUA ZA AWALI HATUJAINGIA MKATABA ZINAZOENDELA NI...

“UWEKEZAJI WA DP WORLD NI HATUA ZA AWALI HATUJAINGIA MKATABA ZINAZOENDELA NI PROPAGANDA CHAFU” FATMA

 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Fatma Hassan Toufiq amesema watu wamekuwa wakitumia suala la Uwekezaji wa DP World kwa ajili ya kujipatia umaarufu huku akisisitiza zinazoendelea katika mitandao ni propaganda chafu na zinania ovu yakutaka kuleta mtafaruko katika nchi, hivyo wananchi wazipuuze.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo julai 14, 2023 Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa UWT wa wilaya hiyo.

Amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia umaarufu wao kupotosha jambo la uwekezaji wa DP World na kudai Bunge lilipitisha makubaliano ya awali ya uwekezaji wanchi ya Dubai Pamoja na Tanzania na si kuingia Mkataba na nchi hiyo.

Pia amewaeleza kuwa Bandari haijauzwa kama wapotoshaji wanavyoendesha Propaganda Chafu badala yake Serikali inataka kufanya uwekezaji Mkubwa ili kuleta tija Mapato ambayo yatasaidia Maendeleo ya Taifa.

‘’Ikumbukwe kwamba Kulikuwa na Wawekezaji wengine ambao Muda Wao Umeisha,Hivyo tumuunge Mkono Mh Rais kwani ana nia Njema ya Kuleta Maendeleo Endelevu katika nchi yetu,’’ameongeza kwa kusema Toufiq.

Previous articleDKT. MAGEMBE AKOSHWA NA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA
Next articlePROF. MDOE AWATAKA WALIMU WAKUU NA WARATIBU KUWASAIDIA WANAFUNZI KUSHIRIKI MASHINDANO YA UANDISHI WA INSHA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here