NA JOSEA SINKALA, MBEYA.
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mbeya Vijijini (kichama) kupitia Mwenyekiti wake Festo Amanyisye Mbilike, umemshukuru Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza kwa kuendelea kuishawishi Serikali kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo jimboni humo.
Jumuiya hiyo ya Vijana chini ya Mwenyekiti Mbilike na katibu wake Japhet Siulanga, imesema haijawahi kutokea Serikali kutoa miradi mikubwa katika jimbo la Mbeya vijijini kama awamu hii (6) chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Haya yote yanafanyika kwa wingi miradi inakuja Barabara zinajengwa, Maji yanasambazwa, umeme, elimu, Afya, kwenye Kilimo nk.. sababu ni ushirikiano mkubwa wa Mbunge wetu (Oran Njeza) na Wabunge wenzake wa Mkoa wa Mbeya”, Mkiti UVCCM Mbeya Vijijini Festo Mbilike.
Kiongozi huyo ameahidi kuendelea kusema kwa wananchi ili wajue Serikali inavyowatumikia kwa kutekeleza miradi mbalimbali.
“Tunajionea kwa macho kinachoendelea Jimboni kwetu (Mbeya vijijini), kwa asilimia kubwa kilichobaki ni kusema tu kwa wananchi nini kinafanyika kwa sasa ili wananchi waliokiamini Chama Cha Mapinduzi wajue”, Festo Amanyisye Mbilike, Mkiti UVCCM Wilaya ya Mbeya vijijini.
“Kwa muda wa miaka aliyohudumu Mhe. Oran Njeza (Mbunge Mbeya vijijini) amekuwa na ushawishi wa kuiomba Serikali kutuona na kutuletea maendeleo na Serikali yetu sikivu imekuwa ikileta miradi mingi sana jimboni. Kilichobaki ni kuisemea tu, kukaa kwetu kimya bila kusema ndio wapinzani husema wao ndio wanaileta”, Mkiti UVCCM Mbeya Vijijini.
Hata hivyo amesema kukaa kimya ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii ni kutomtendea haki Mbunge wa Mbeya vijijini anayeshirikiana na wenzake kuishawishi Serikali kutafuta na kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo mkoani Mbeya hivyo kuwataka Madiwani kuendelea kusema katika maeneo yao juu ya mambo yanayofanyika.