UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa waiomba serikali kupitia wizara ya kilimo nchini kuvipandisha hadhi vyuo vya kilimo vikiwemo vilivyoanzishwa na waasisi wa taifa ikiwa ni njia mojawapo ya kuikuza sekta ya kilimo nchini.
Maombi hayo yalitolewa na mwenyekiti wa UVCCM taifa Ally Mohamed Kawaida jana akiwa katika ziara ya ukaguzi wa programu ya Jengaa Kesho Bora(BBT) katika chuo cha kilimo MATI-MARUKU kilichopo mkoani kagera.
“Niliposhuka Mwanza juzi nikatembelea chuo cha MATI-UKIRIGURU kilianzishwa mwaka 1939 chakushangaza chuo kile bado kinatoa elimu ya stashada na astashahada ya kilimo tukapata wazo jumuiya ya vijana kumbe inawezekana tukawa na chuo cha kilimo kanda ya ziwa, tukishuka hapa katikati tunacho SUA kilichopo Morogoro na huku chini tukawa na chuo cha Mbeya tukawa na vyuo walau vitatu, tuiombe wizara ya kilimo kwa kukiangalia chuo chetu kile cha Mwanza ili kwa vijana wenzetu waliopo kanda ya ziwa nao wasisafiri masafa ya mbali kukifuata chuo cha kilimo Morogoro”
Naye mkuu wa chuo cha MATI- MARUKU, Luhembe Mathew wakati akitoa soma taarifa yake alisema kuwa chuo hicho kilipokea wanafunzi 39 ambao ni wanufaika wa hiyo kufikia sasa wameweza kupata mafunzo ya kilimo kwa vitendo na nadharia.