Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Charles Msonde amewataka wazazi,walezi na jamii kushirikiana kikamilifu na walimu katika Malezi na Usalama wa Watoto.
Dkt.Msonde ameyasema hayo jana Septemba 8,2023 Jijini Dodoma,wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Waratibu wa Mpango wa Shule salama na wasimamizi wa usalama wa jamii wa Mikoa na Halmashauri.
“Malezi na ulinzi wa Mtoto ni jukumu letu sote hivyo Wazazi,walezi na jamii shirikianeni na Shule katika kuhakikisha mnawalinda watoto na kuwakinga dhidi ya ukatili katika jamii , msiwaachie jukumu hilo walimu pekee kwani mtoto anaweza kupata changamoto Nyumbani,kwenye jamii ama shuleni hivyo ni muhimu kuwalinda kwa pamoja,”amesema Msonde
Amesema Malezi ya watoto ni jambo la muhimu ndani ya jamii hivyo ni wajibu wa walimu kuhakikisha watoto wanapata malezi bora kwa kuhakikisaha kila siku wapo katika mazingira salama