Kambi ya upinzani bungeni nchini Uganda imepinga bajeti ya shilingi Milioni 350 Ush sawa na Milioni 220.6 Tsh iliyotengwa kwa ajili ya manunuzi ya mavazi ya Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Katika bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kajaida, Tsh Bilioni 150.6 zimetengwa kwa ajili ya Ikulu ambapo Tsh Milioni 220.6 ni kwa ajili ya manunuzi ya mavazi ya Rais.
Akipinga bajeti hiyo,Mbunge wa Kira Municipality Ibrahim Ssemujju Nganda amesema “kuna Ush.Milioni 350 kununua nguo,kiasi kilekile kilipatikana mwaka jana.Hii inamanisha tunatumia wastani wa Ush.Milioni moja kwa ajili ya mavazi ya Rais.
Upinzani nchini humo (Uganda) wapendekeza bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Ikulu kupunguzwa kutoka Ush.Bilioni 150 hadi Ush.Bilioni 51.6
Chanzo.Daily Monitor (Uganda)