Home KITAIFA UONGOZI WA MACHINGA IRINGA WAJIUZULU KUFUATIA SHINIKIZO LA VIONGOZI WA SERIKALI

UONGOZI WA MACHINGA IRINGA WAJIUZULU KUFUATIA SHINIKIZO LA VIONGOZI WA SERIKALI

Na Dishon linus

Sakata la machinga mjini Iringa limeendelea kuwa na taswira mpya mara baada ya mwenyekiti na katibu wa umoja wa machinga Iringa wameamua kutangaza kujiuzulu nafasi zao, katika kile walichosema ni viongozi serikali kuwaona wao ndio chanzo cha migomo ya machinga Iringa tangu kuanza kwa utekelezaji wa kuwaondoa machinga katikati ya mji.

Katika taarifa ya pamoja kati ya Yahaya Mpelembwa na Joseph Mwanakijiji wamesema

“Ili kulinda heshima zetu na kuruhusu utawala wa sheria tunaachia nafasi zetu na kuruhusu utawala wa sheria hivyo basi tunaachia ngazi kwa maslahi mapana ya wamachinga Iringa”

Wawili hao wameeleza kuwa, sababu za msingi kufikia maamuzi hayo ni kwamba wamejiridhisha na yanayoendelea katika migomo na vurugu ndani ya manisipaa ya Iringa dhidi ya machinga wanaodai haki zao, kuwa wao viongozi ndio wanalalamikiwa kuwa chanzo cha migomo hiyo.

Kwenye barua yao Yahaya Mpelembwa na Joseph Mwanakijiji hawajaeleza ni viongozi gani wa serikali waliowatuhumu kwenye sakata hilo la migomo.

Hivi karibuni wamachinga walifunga barabara ya Samora Mlandege na Ipogolo wakishinikiza manispaa ya Iringa kutimiza matakwa yao katika soko jipya la Mlandege,mojawapo ya shinikizo lao ni mansipaa kushindwa kuleta kituo cha bajaji eneo soko hilo

Tukio hilo linapelekea wamachinga hao wa soko la Mlandege kutangaza kurudi kwenye maeneo ya awali walioondolewa awali na serikali hoja kubwa ikiwa ni uongozi wa manispaa kushindwa kuimarisha huduma za kijamii kwenye soko hilo.

Previous articleTAMASHA LA SIMBA DAY UNYAMA KAMA WOTE… RAIS AKOSHWA NA KIBEGI _ MAGAZETINI LEO JUMATATU AGOSTI 07/2023
Next articleWATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI PINDI WATOAPO HUDUMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here