Home MICHEZO UONGOZI WA KLABU YA YANGA SC WAPANGA KUISHTAKI SIMBA SC

UONGOZI WA KLABU YA YANGA SC WAPANGA KUISHTAKI SIMBA SC

 

Na Dishon Linus.

 

Klabu ya Yanga imepanga kuwasilisha barua ya malalamiko na kuomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya mashabiki waliovalia jezi za kalbu ya Simba walioonekana kwenye video wakimshambulia shabiki aliyevalia jezi ya Yanga katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi wa sheria wa Yanga Simon Patrick amesema kitendo hiko sio cha kiungwana Simba na Yanga ni watani na sio maadui na kuomba mamlaka husika ziweze kuchukua hatua kali kwa wote waliojusika na kitendo hiko.

 

“Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisaa, hakuna sababu ya msingi ya kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni watani wa jadi sio maadui”.

 

“Naiomba bodi ya ligi kuu, shirikisho la Soka nchini (TFF), jeshi la polisi wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe. Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi, na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama” ameandika Simon Patrick katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Previous articleBALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA
Next articlePOLISI SONGWE YAKEMEA ULEVI KUEPUKANA NA AJALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here