Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko amesema kuwa Uongozi si kama shati kwamba Kila mtu anaweza kuvaa badala yake amesema kiongozi anapikwa na kujengwa.
Hivyo amewataka wanatanga kuhakikisha wanachagua viongozi wenye uwezo kutoka chama Cha Mapinduzi CCM hasa wanawake katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani .
Hayo ameyasema wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilan ya ccm katika kata tano za Pongwe,Mabawa,Tongoni,Mwanzange na Maweni zilizopo katika jiji Tanga.
” Viongozi wazuri wanapatikana ndani ya chama Cha mapinduzi hivyo msifanye makosa utakapofika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu” Amesema sekiboko.