Home KITAIFA UKOSEFU WA HUDUMA YA AFYA YA AKILI YACHANGIA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI

UKOSEFU WA HUDUMA YA AFYA YA AKILI YACHANGIA PICHA ZA UTUPU MITANDAONI

 

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema ukosefu wa huduma ya afya ya akili hupelekea mmonyoko wa maadili ikiwemo kujirekodi na kutuma picha au video za utupu mitandaoni.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo agosti 30, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa robo mwaka wa Wadau wa Ustawi wa Jamii.

Amesema Vitendo hivyo vinaweza kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo madhara kimwili, kafya, kisaikolojia na kiuchumi na kuongeza kuwa Vitendo hivyo.

Pia vimeendelea kutokea katika nchi zote duniani zilizoendelea na zinazoendelea ikiwemo Tanzania ambapo vinasababisha madhara makubwa kwa mtu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amesema Vitendo vya ukatili vinaathiri ukuaji wa watoto na vinasababisha nguvu kazi dhaifu isiyokuwa na tija ya kutosha katika Taifa kwa siku za usoni.

“Sisi sote tumekuwa tukisikia matukio mbalimbali ya watu kudhuru wengine au wao wenyewe kujidhuru kutokana na msongo wa mawazo, Hivi karibuni kumetokea tukio la kusikitisha mkoani Arusha kuhusu mama kujinyonga kwa kushindwa kurejesha mkopo,’’
‘’Hivyo, niwaombe wadau na maafisa Ustawi wa Jamii tubuni njia mbadala ya kuwasaidia na kutoa elimu kwa wanawake wanaojiingiza kwenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi zinazohusisha mikopo mbalimbali ili kuwaepusha na madhara makubwa yanayopelekea hadi wengine kupoteza uhai na kuacha familia katika mazingira hatarishi,”amesema Dkt. Gwajima.

Licha ya hayo amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwamo mila na desturi potofu zinazopelekea ukatili katika jamii, serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na hizo ni Kuanzishwa kwa Mfumo Jumuishi wa Kitaifa wa Kushughulikia Mashauri ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi nchini.

Previous articleWANAOWEKA PICHA ZA KUDHALILISHA MITANDAONI WAONYWA.
Next articleSERIKALI KUENDELEA KUJIKITA KUONGEZA BAJETI YA KILIMO NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MASOKO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here