Home KITAIFA UJENZI NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME IRINGA, MBEYA HADI RUKWA KUANZA JUNI 2023...

UJENZI NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME IRINGA, MBEYA HADI RUKWA KUANZA JUNI 2023 – 2025.

 

NA SAIDA ISSA, DODOMA.

Serikali imesema mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 620 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma unatarajiwa kuanza Juni 2023 na kukamilika mwezi
Septemba 2025.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Ujenzi wa umeme wa kilovoti 400 kutoka Iringa – Mbeya – Tunduma –Sumbawanga utaanza pamoja na kuwalipa fidia Wananchi waliopitiwa na laini hiyo.

“Mradi huu unalenga kuunganisha Gridi ya Taifa na nchi za Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool – SAPP) na utagharimu jumla ya Shilingi trilioni 1.38,” Amesema Naibu wa Nishati.

Aidha amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari imetoa Shilingi bilioni 16.43 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi 6,500 wanaopisha mradi na kazi ya ulipaji fidia imekamilika kwa awamu ya kwanza ambapo Wananchi 4,750 wamepokea Shilingi bilioni 13.67 na maandalizi ya awamu ya pili yanaendelea na malipo yanatarajiwa kufanyika ifikapo Julai 2023.

Previous articleBARABARA ZA MJI WA MOMBO ZAENDELEA KUIMARISHWA KUPITIA TARURA
Next articleNEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO UDIWANI KATA 14 _ MAGEZITINI LEO ALHAMISI JUNI 15/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here