Home KITAIFA UJENZI DARAJA LA MTO PANGANI KUANZA HIVI KARIBUNI

UJENZI DARAJA LA MTO PANGANI KUANZA HIVI KARIBUNI

Serikali imesema Mkandarasi tayari yupo site kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Daraja la kihistoria la Mto Pangani lenye urefu wa Mita 525, litakalounganisha Barabara ya Tanga – Pangani hadi Bagamoyo Mkoani Pwani kupitia Saadani (Tanga – Pangani – Saadan – Bagamoyo).

Akitoa taarifa kuhusu kuanza rasmi kwa ujenzi wa Daraja hilo, Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amesema Barabara zinazojengwa pamoja na Daraja hilo vinatarajiwa kupunguza muda wa kusafiri kwenda Jijini Tanga ambapo Daraja hilo hadi kukamilika litagharimu Tsh. Bilioni 82.19 na mpaka sasa Mkandarasi tayari amelipwa Tsh. Bilioni 11.86.

 

 

“Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo Africa (ADB) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi Shandong Luqiao Group Limited, na Mhandisi Mshauri Leah International kwa kushirikiana na Leah Associates”

Mradi huu umeanza December 07, 2022 na unatarajiwa kukamilika December 07, 2025 ambapo utatekelezwa ndani ya miezi 36 na utakuwa chini ya matazamio ndani ya miezi mingine 36.

 

Awamu hii ya mradi (LOT 2) inahusisha pia ujenzi wa Barabara kiwango cha lami KM 25.6 ambapo KM 14.3 ni Barabara kutoka Bweni kwenda Tungamaa, KM 5.9 Barabara ya Utalii kwenda Ushongo na KM 5.4 Barabara za Mitaa Pangani Mjini.

Previous articleDKT. ANETH ASISITIZA MATUMIZI YA VITABU VYENYE ITHIBATI
Next articleDIRA YA MAENDELEO YAIBADILISHA NCHI ◾ UMASKINI WAPUNGUA ,KASI YA UCHUMI, UMRI WA KUISHI VYAONGEZEKA : MAGAZETINI LEO JUMANNE APRILI 04/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here