Takwimu zinaonesha kuwa kumekua na ongezeko la wagonjwa wanaosumbuliwa na Shinikizo la juu la damu kutoka wagonjwa 688,901 kwa mwaka 2017 hadi kufikia wagonjwa 1,345,847 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la 95.4℅ katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Mei 17/2023 wakati akizungumza na waandishi wa babari katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma,ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani.
“Takwimu zinaonyesha kuwa watu 3-4 kati ya 10 wana shinikizo la juu la damu kwa uchunguzi uliofanywa kwenye mikoa ya Pwani,Arusha,Geita,Mtwara,Lindi,Zanzibar,Iringa na Dar es salaam.”. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
“Wizara imeruhusu dawa za kukabiliana na shinikizo la juu la damu katika ngazi ya msingi kwa kuruhusu dawa tatu(3)ambazo ni Losartan,Amplodipine na Hydralazine kutumika katika ngazi ya kituo cha afya na dawa mbili (2) ambazo ni Nifedipine na Frusemide ambazo hutumika katika ngazi ya Zahanati”. Waziri Ummy Mwalimu