Home KITAIFA UFAFANUZI WA KLINIKI ZA MADAKTARI BINGWA BAADA YA SAA ZA KAZI WATOLEWA

UFAFANUZI WA KLINIKI ZA MADAKTARI BINGWA BAADA YA SAA ZA KAZI WATOLEWA

 

“Utaratibu wa kutoa huduma za afya binafsi baada ya masaa ya kazi sio jambo jipya” amesema Waziri Ummy na kuongezea kuwa utaratibu huo umekuwa ukifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Mifupa MOI na Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Waziri Ummy amesema kuwa utaratibu huo unasimamiwa na miongozo mahususi iliyopitishwa na bodi za Hospitali husika.

“Muhimbili utaratibu huu Muhimbili wanauita Intramural Private Practice at Muhimbili, (IPPM), Wizara inaona kwamba ni jambo lenye tija kushusha utaratibu huu kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa” ameeleza Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema utaratibu huo utawezesha wananchi kuhudumiwa kwa haraka lakini kwa kulipia kwa ziada, kuwatuliza madaktari kwenye vituo vyao vya kazi pamoja na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo vingine vya kazi ‘vijiwe’ baada ya muda wa kazi.

“Zoezi hili haliendi kuathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi badala yake linakwenda kuboresha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa wananchi katika maeneo yao.

“Utaratibu huu unalenga kuhakikisha tunavutia madaktari bingwa kufanya kazi mikoani, tumetangaza nafasi za madaktari bingwa 35 mwezi Juni 2023 wakaomba madaktari 15, 11 walikidhi vigezo, wakaripoti madaktari bingwa 6 tuu”

Waziri Ummy amesema ni wajibu wa Serikali kuweka mazingira ya kuvutia madaktari bingwa kufanya kazi katika hospitali za umma.

Amesema kuwa utaratibu huo utazinufaisha Hospitali kwa kuongeza mapato kwakuwa watu wanaofika kwenye kliniki binafsi watalipia kwa gharama ya juu tofauti na wale wa muda wa kazi za mwajiri.

Previous articleIGP WAMBURA APOKEA TUZO KUTOKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NCHINI
Next articleZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 10 KUWEKEZWA KATIKA BIASHARA YA KABONI NCHINI TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here