Home KITAIFA UFAFANUZI KUHUSU KINACHODAIWA MTOTO KUGEUKA JIWE WILAYANI MUSOMA

UFAFANUZI KUHUSU KINACHODAIWA MTOTO KUGEUKA JIWE WILAYANI MUSOMA

 

 

Taarifa ya uchunguzi iliyofanywa imethibitisha bila shaka kuwa HAKUNA MTOTO ALIYEGEUKA KUWA JIWE wilayani Musoma mkoani Mara.

Bi. Amina Abdala mkazi wa Katoro Chato alihamia kijiji cha Mwabuki Bariadi akijishughulisha na biashara ya kuuza Pombe za kienyeji, kuhudumia vinywaji kwenye Bar na wakati mwingine mhudumu wa nyumba za kulala wageni. Tarehe 27/3/2023 alijifungua mtoto wa kike kwenye Zahanati ya Mwabuki akiwa ni mtoto wake 3 aliozaa na wanaume tofauti( kila mtoto na baba yake).

Mtoto wa tatu alizaa na Hamisi mwenye makazi Mungaranjabo, Buhare hapa Musoma. Bi. Amina alimuahidi kumzalia mtoto wa kiume Hamisi lakini kwa bahati mbaya mtoto aliyezaliwa alikuwa wa kike.

Hamisi yupo Dar es Salaam na alituma nauli ili watoto wapelekwe kwa bibi yao Buhare Musoma.

Bi Amina alianza safari tarehe 19/3/2023 akiaga anaenda Mwanza kwenye msiba wa mama yake lakini alipofika Bariadi akapanda basi la Musoma akiwa na jiwe alilolichukuwa kwenye mawe ya ujenzi wa nyumba ya mzee Mirembe wa Mwabuki alikokuwa anaishi.

Alifika Musoma saa 3.00 usiku na kupokelewa na wenyeji wake na kuzusha mtoto pacha aitwae Amiri ameguka jiwe na kutaka azikwe usiku huohuo ili kuondoa mikosi.

HOJA YA MTOTO KUGEUKA JIWE.

Kamati imerijiridisha kuwa Amina alikuwa na makubaliano na Hamisi ya kumzalia mtoto wa kiume tangu mwanzo wa mahusiano yao hivyo Hamisi akaendelea kukea mimba akitarajia mtoto wa kiume.

Baada ya kujifungua mtoto wa kike, Bi Amina aliendelea kumwaminisha Hamisi kuwa amejifungua pacha wa kike na kiume.

Pia hali duni ya maisha ya Amina kuhudumia familia ya watoto watatu ilichangia kusema uongo huo.

Previous articleMENEJA TANROADS KIGOMA: KILOMETA 420 ZA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI KUJENGWA KWA MARA MOJA, HAIJAWAHI KUTOKEA
Next articleRAIS DKT. SAMIA: TUMEPITIA WAKATI MGUMU KUFIKIA UMOJA NA MSHIKAMANO _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI APRILI 23/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here