Home KITAIFA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO WAMALIZIKA SAME

UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO WAMALIZIKA SAME

Uchaguzi mdogo wa marudio katika kata mbili za Njoro na Kalemawe halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro umemalizika na tayari matokeo yametangazwa na kupatikana viongozi wapya watakao ongoza kata hizo mpaka utakapo fanyika uchaguzi mwingine.

Kwenye kata ya Kalemawe Mgombea wa chama cha Mapinduzi CCM Jofrey Mtwa Jofrey ametangazwa mshindi kwa kupata jumla ya kura 1286 sawa na asilimia 90.5 ya kura zote na kata ya Njoro pia Mgombea wa CCM Omary Abdallah ameshinda kwa kupata kura 981 sawa na asilimia 91.7 ya kura zote.

Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema hakukuwa na changamoto yoyote muda wote wa zoezi hilo akisema amejiridhisha kwa kupita katibu vituo vyote kuangalia hali ya usalama na kujiridhisha wananchi wametimiza haki ya kikatiba kushiriki uchaguzi bila changamoto yoyote.

Previous articleMCHECHU ATANGAZA KIAMA CHA MASHIRIKA MZIGO KWA SERIKALI _ MAGAZETINI LEO IJUMAA JULAI 14/2023
Next articleLUIS MIQUISSONE (KONDE BOY) AMEMALIZANA NA SIMBA SC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here