Home KITAIFA UBANGUAJI WA KOROSHO NCHINI CHANZO CHA ONGEZEKO LA FURSA ZA AJIRA

UBANGUAJI WA KOROSHO NCHINI CHANZO CHA ONGEZEKO LA FURSA ZA AJIRA

UBANGUAJI WA KOROSHO NCHINI CHANZO CHA ONGEZEKO LA FURSA ZA AJIR

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kuwa hali ya ubanguaji korosho Nchini sio ya kuridhisha kwasababu iko chini ya asilimia 10 ya korosho ghafi zinazozalishwa.

Ameyazungumza hayo leo September 2,2023 kwenye kilele cha mashindano ya mbio za Korosho Marathon yaliyofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani ambayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa.

Pia amesema ubanguaji wa korosho nchini unafaida nyingi ikiwemo kuongeza vyanzo vya mapato kwa wadau na wakulima, kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa viwanda nchini.

“Ganda la korosho zilizo banguliwa hutumika kuzalisha mafuta yanayotumika katika mitambo kama kilainishi.

Kanali Abbas pia amewataka wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho wahakikishe viwanda vyao vinafanya kazi ya ubanguaji kama vibali vyao vya umiliki vinavyo eleza.

Previous articleDC ILEJE AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA MAPOKEZI YA MWENGE
Next articleSEKTA YA POSTA KUIKOMBOA AFRIKA KIUCHUMI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here