Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt.Abel Nyamahanga amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ndani ya siku tatu kufika ofisi kwake kutoa taarifa kamili ya ujenzi wa shule ya sekondari Mafumbo iliyojengwa chini ya kiwango.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 470 ilihali thamani vyumba vya madarasa vilivyojengwa havilingani na gharama zilizotumika.
Dkt.Nyamahanga ameongeza kwa kusema kuwa hali hiyo imechangia kuongezeka kwa changamoto kwa baadhi ya wahandisi kujenga miradi chini ya kiwango.
“Tunakuahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika kuhujumu ujenzi wa mradi wa shule ya sekondari Mafumbo” Justus Magongo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.