WAGANGA wa tiba asili na tiba mbadala Tanzania wamemwomba IGP Camillius Wambura kuingilia kati changamoto sita zinazowakabili ikiwemo kutapeliwa mara kwa mara kwa njia ya mtandao kupitia mwamvuli wa jeshi la polisi.
Akisoma risala kwa niaba ya Waganga hao wakati wa halfa ya kufunga mafunzo ya kuinua ubora wa tiba asili na tiba mbadala yaliyoratibiwa na Wizara ya afya iliyofanyika julai 1, 2023 jijini Dodoma Mussa Daud amesema changamoto wanayokutananayo ni kutapeliwa kwa njia ya kumiwa ujumbe mfupi ukiomba fedha ambao unaanza tuma kwenye namba hii hali hupelekea kutuma hela sehemu ambayo siyo sahihi nakujikuta wametapeliwa.
‘’Jeshi la polisi lishirikiane na UWAWATA katika kuhakikisha tunapambana na matapeli wanaotumia mwamvuli wa tiba Asili na Tiba Mbadala , hii ni kwa ajili ya kukomesha wizi wa mtandao kwa waganga na kwa wale wote wanaotumia mwamvuli wa jeshi la polisi ikiwa wao si askari polisi,’’ amesema Daudi.
Pia amebainisha changamoto nyingine ni Pamoja na Waganga kukamatwa ovyo kulingana na mwonekano wao (Mavazi na viashiria mbalimbali mfano shanga).
Kwa upande wake Mwakilishi wa IGP Kamishna wa Kamisheni ya polisi jamii Faustine Shigolile amekili kuwepo kwa changamoto hiyo huku akidai mfarifu mmoja hutuma ujumbe mfupi kwa Zaidi ya 30 nahumpatia zaidi ya milioni moja nakushauri kuwa makini wakati wa utumaji wa pesa.
‘’Mfano wa jumbe zinazotumwa kutoka jeshi la polisi kupitia makampuni ya simu za kiganjani ni Pamoja na ‘’usifuate maelekezo kuhusu huduma unazozitumia kutoka kwenye namba usiyoifahamu, usikubali kutapeliwa , usitume pesa kwa mtu usiyemfahamu bila kuhakiki,’’amesema CP Faustine Shilogile.
Akizungumzia Sakata la lambalamba na Kamchape katibu wa Umoja wa Waganga wa Tiba asili na Wakunga Tanzania (UWAWATA) Lucas Mlipu amesema wao hawatokubali kutumiwa nawatu hao kwa manufaa yao wenyewe na kuliomba jeshi la polisi kuwa karibu nao ili kuweza kuwafichua wahalifu wanaojiita lambalamba kwakuwa wamekuwa kikanzo na kuharibu sifa ya waganga.
‘’Jamii ielimishwe juu ya madhara ya Rambaramba na kamchape na waelimishaji wawe waganga wenye taaluma asili ya tiba asili kwa lengo la kuelimisha jamii tofauti baina ya tiba asili na matapeli wanaotumia mwamvuli wa Tiba Asili,’’ amesema Mlipu.
,………………………