Home KITAIFA TSH. MIL 800 KUTUMIKA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI BUNDA

TSH. MIL 800 KUTUMIKA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI BUNDA

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Milioni 800 kwa mwaka 2023/24 pamoja na kuondoa Mita zaidi ya Elfu 6 zilizochakaa kutokana na kutumika kwa zaidi ya miaka 10 ili kudhibiti upotevu wa maji ambao ni asilimia 36 ya Lita milioni 3.8 za Maji yanayozalishwa kwa siku.

Akizungumza na waandishi wa habari julai 20,2023 Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (BUWSSA), Esther Gilyoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya BUWSSA na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema upotevu wa Maji Bunda Mkoa wa Mara kwa mwaka 2022/2023 umefika asilimia 36%

“Mkakati huu ambao tunao najua itaenda kutokomeza kabisa upotevu wa maji katika Wilaya ya Bunda, hivyo wananchi waendelee kutunza miradi yetu ya maji”,amesema

Gilyoma amesema Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imeandaa andiko la mradi kwaajili ya kukopa kuhakikisha upotevu wa Maji unapungua kwa kiasi kikubwa zaidi.

“Tumeandaa andiko kwaajili ya kukopa fedha kiasi cha Shilingi 815,000,0000 ili upotevu wa maji upungue kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024”.Amesema Gilyoma

Hata hivyo amesema Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Bunda haina huduma ya Majitaka, hivyo Magari ya Watu binafsi ambayo yanasimamiwa na halmashauri ya Mji wa Bunda ndiyo yatatumika katika kutoa huduma.

Previous articleKITUO KIPYA CHA AFYA MAKOWO CHAANZA KUTOA HUDUMA,MTOTO WA KWANZA KUZALIWA AITWA SAMIA
Next articleNAIBU WAZIRI NDERIANANGA AGAWA MITUNGI YA GESI ROMBO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here