Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki amewaagiza maofisa utumishi na makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kuhakikisha wanafuatilia walimu ambao hawajapandishwa vyeo kwa muda mrefu.
Pia ameagiza kuhakikisha kuwa madai ya walimu wote ikiwemo malimbikizo ya mishahara yanaingizwa katika mamlaka husika na kufuatilia madai ya malimbikizo ya fedha za likizo na uhamisho.
“Naomba muende mkawe na mawasiliano mazuri katika utendaji wenu wa kazi ikiwemo kutumia lugha za staha kwa walimu pale wanapoleta changamoto zao,”amesema.