Home KITAIFA TPSF ,UDSM YA SAINI MOU MWAROBAINI AJIRA ZA WAHITIMU WA VYUO

TPSF ,UDSM YA SAINI MOU MWAROBAINI AJIRA ZA WAHITIMU WA VYUO

 

Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeingia mkataba wa makubaliano na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi Kiuchumi (HEET) ili kuwajengea uzoefu wahitimu pindi wanapoingia kwenye mfumo wa ajira hivyo kukabiliana na changamoto ya ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu nchini.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPSF Bw. Raphael Maganga alizielezea takwimu za wanafunzi ambao hawana ajira na namna mradi huo utakavyo wasaidia.

“Zaidi ya wanafunzi 800,000 hadi milioni moja wanahitimu kila mwaka, kati yao chini ya asilimia 15 wanaajiriwa kwenye ajira rasmi. Makubaliano haya kati ya UDSM na TPSF yanalenga kutatua changamoto hii kwa kuangalia ni jinsi gani Sekta Binafsi itaweza kuajiri wahitimu wengi na Vyuo kuwa na mitahala inayoenda na mahitaji na mabadiliko ya biashara” alisema Bw. Maganga.

Aidha Mgeni rasmi, Prof. Carolyne Nombo; Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alisema mradi huu wa HEET licha ya kuwa utasaidia kuongeza uzoefu kwa wahitimu pia utatumika katika maboresho ya mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira.

“Kumekua na changamoto kwa wahitimu ambao wanatoka katika vyuo vyetu, wengi wanaujuzi lakini ujuzi huu hauwawezeshi kuingia kazini moja kwa moja kwahio tumeona njia bora ya kutatua changamoto hii nikuhakikisha vyuo vyetu vinakua na mahusiano na waajiri ilikufahamu mahitaji ya soko la ajira na zalisha wahitimu wanao kidhi mahitaji hayo” alisisitiza Prof. Nombo.

Makamo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye alielezea namna mradi wa HEET utakavyoendana na mahitaji ya soko la ajira nchini.

“Tunataka pia hii mikataba iweze kuwafanya wahitimu wetu wafikirie kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa lakini pia kupitia hii mikataba tuweze kutoa ule ujuzi tulionao kusaidia taasisi ambazo tumeingia nazo mkataba” alizungimza Prof. Anagisye.

Mradi wa HEET unafadhiliwa na benki ya dunia lengo lake kuu ni kuboresha utoaji wa elimu ya juu ilikuzalisha wahitimu wanao endana na mahitaji ya soko.

Previous articleWAZIRI MHAGAMA AKABIDHIWA KIPANDE CHA SEHEMU YA UJENZI WA UWANJA WA MASHUJAA
Next articleKIKONGWE AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here